CCM YAINGILIA KATI MSONGAMANO WA MAGARI UNGUJA

                                     Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeingilia kati kadhia ya msongamano na foleni za magari katika Mji wa Unguja na kuwataka wananchi wawe wavumilivu kwani maagizo ya kukabiliana na hali hiyo yameshatolewa kwa wizara husika na wadau wengine.

Akizungumza Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui leo 06 Mei 2026, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi na Uenezi, Komredi Khamis Mbeto Khamis alisema wameitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuwasimamia  wakandarasi ili waweke njia mbadala katika baadhi ya maeneo.

" Wakandarasi wameagizwa katika baadhi ya maeneo kuweka njia mbadala za muda" alisema Mwenezi Mbeto.

Alisema katika baadhi ya maeneo wamefanya hivyo na pia kuna njia ambapo gari zinatumia upande mmoja wa barabara.

"Unajua unapotaka kujenga kuna mambo lazima yatakugusa hivyo wananchi wawe wavumilivu baada ya muda si mrefu yatakaa sawa" alisema Mwenezi Mbeto.

Komredi Mbeto pia amewataka wananchi na watumiaji wa barabara kuchukua taadhari zikiwemo za mazingira kipindi hiki mvua zinaendelea kunyesha.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja Unguja na Pemba.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA