BILIONEA WA ABERCROMBIE & KENT KUWEKEZA ZAIDI NCHINI



                                  Na Mwandishi Wetu Port Said, Misri

BILIONEA na mmiliki wa moja ya kampuni kubwa zaidi Duniani katika biashara ya utalii ya Abercrombie and Kent, Manfred Lefebvre amesifu maendeleo ya sekta ya utalii nchini Tanzania na kuahidi kuwekeza zaidi nchini.

Bilionea Manfred ameyasema hayo katika mazungumzo leo Ijumaa 08 Mei 2026 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi, pembeni mwa Mkutano wa Viongozi wa Sekta unaofanyika ndani ya meli ya kitalii ya Bilionea huyo ambayo leo inaendelea na safiri kutoka Bandari ya Port Said kwenda Alexandria. 

“Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo naziona zikiendelea vyema katika sekta ya utalii barani Afrika. Nauona uongozi wa sasa ukiweka mbele utalii sana hasa chini ya Rais Mama Samia,” alisema Manfred ambaye miaka minne iliyopita pia alihudhuria uzinduzi wa filamu ya “Tanzania: The Royal Tour,” jijini New York, Marekani. 

Kampuni ya Abercrombie and Kent tayari imewekeza Tanzania ikileta maelfu ya watalii wakiwemo wale wanaofika nchini kupitia meli zao za kitalii chini ya kampuni tanzu ya Crystal Cruises ambazo huvinjari mara kadhaa Zanzibar, Kilwa na Dar es Salaam. 

Kwa upande wake Dkt. Abbasi alimhakikisha ushirikiano na Serikali katika hatua zake zote zijazo za kuongeza wigo wa uwekezaji wake nchini Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA