BALOZI KAGANDA RASMI MAJUKUMU MAPYA JAMHURI YA KOREA
Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Korea, Mhe. Noel Emmanuel Kaganda, amewasili jijini Seoul, Korea tayari kuanza kazi rasmi.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon, Balozi Kaganda alipokelewa na Mkuu wa Ofisi ya Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Korea Bw. Kang Jin Hyun pamoja na wawakilishi wa Kundi la Mabalozi wa Afrika (African Group of Ambassadors AGA) nchini Korea, akiwemo Naibu Balozi wa Zambia Bi. Wray M. Hamweene; Bw. Claude K. Ganza pamoja na maafisa wa Ubalozi.
Wawakilishi wa Kundi la Mabalozi wa Afrika (AGA) nchini Korea walimkaribisha Balozi Kaganda nchini Korea na kumtakia heri katika utekelezaji wa majukumu yake mapya na kumsisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano na mshikamano kati ya nchi za Afrika nchini Korea.
Aidha, Mhe. Balozi alishukuru kwa mapokezi aliyopatiwa na kuahidi kushirikiana kwa karibu na balozi mbalimbali za Afrika kuendeleza urafiki, ushirikiano na mahusiano yenye manufaa ya pamoja. 🇹🇿🇰🇷

.jpg)
Comments
Post a Comment