TISEZA, TPSF WATEMBELEA UJENZI UWANJA WA AFCON 2027 ARUSHA
Mkurugenzi wa Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Bw. Gilead Teri kwa kushirikiana na Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) pamoja na ujumbe wa wawekezaji, walifanya ziara ya kutembelea uwanja wa mpira unaoendelea kujengwa jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya AFCON 2027.
Ziara hiyo ililenga kujadili na kuchambua kwa kina fursa mbalimbali za uwekezaji zitakazojitokeza kabla, wakati na baada ya mashindano ya AFCON 2027. Kupitia majadiliano hayo, msisitizo uliwekwa katika namna bora ya kuvutia wawekezaji na kuendeleza uwekezaji nchini, huku jukwaa la mashindano hayo makubwa ya kimataifa likitumika kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi.
TISEZA inaendelea kujipanga kuhakikisha Tanzania inanufaika kikamilifu na fursa za kiuchumi zitokanazo na AFCON 2027, kwa kuimarisha miundombinu na mazingira rafiki ya uwekezaji.




Comments
Post a Comment