TANZANIA NA MAREKANI KUONGEZA USHIRIKIANO
Na Mwandishi Wetu, Washington D.C
WAZIRI wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, amekutana na kufanya Kikao na Mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Nick Checker, katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Washington D.C nchini Marekani.
Kikao hicho kilifanyika ikiwa ni pembezoni mwa Mkutano wa Kipupwe wa Benki ya Dunia na IMF (2026 IMF/WBG Spring Meetings) inayofanyika, Jijini humo.
Katika hicho baina ya Waziri wa Fedha wa Tanzania Balozi Omar na Mkuu wa Ofisi Masuala ya Afrika Nick Checker kilihusu masuala mbalimbali ya ushirikiano katika maeneo ya kiuchumi kati ya nchi hizo mbili ikiwemo uwekezaji katika sekta ya madini.
Jopo la ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho, lilimjumuisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Natu El-maamry Mwamba.
Wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Aboud Hassan Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Elsie Sia Kanza, Ofisa Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Liz Trobaugh na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.





Comments
Post a Comment