RAIS SAMIA, DKT. MWINYI WAJUMUIKA KUMBUKIZI KIFO CHA HAÝATI RAIS KARUME


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaongoza viongozi wa kitaifa, wanafamilia na wananchi mbalimbali katika dua maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Dua hiyo imefanyika leo, tarehe 07 Aprili 2026, katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar, Mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo pia imehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba,  Mama Fatma Karume na familia yake, Viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya miaka 54 tangu kifo chake.

Baada ya kisomo hicho maalum, Rais Dkt. Mwinyi pamoja na viongozi na wanafamilia walizuru kaburi la Hayati Sheikh Abeid Amani Karume na kuweka mashada ya maua. 

Viongozi wengine waliohudhuria kisomo hicho ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah, Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji George Masaju, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda pamoja na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi.

Rais Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi akishiriki dua maalum ya kumuombea Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Kumbukumbu hiyo imetimiza miaka 54 tangu Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, tangu kifo chake mwaka 1972. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, mara baada ya kuwasili kwenye dua hiyo. Picha Zote na Ikulu, Zanzibar

Aidha, dua hiyo imehitimisha Wiki ya Kuwaenzi na Kuwakumbuka Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar waliotangulia mbele ya haki, ambayo huadhimishwa kitaifa kila mwaka.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA