RAIS MSTAAFU WA ETHIOPIA YUPO NCHINI KIKAZI
RAIS Mstaafu wa Ethiopia, Sahle-Work Zewde amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu hadi hapo Aprili 22, 2026.
Zewde ataungana na Rais Mstaafu wa Liberia, ambaye pia ni Mlezi wa Mtandao wa Wanawake Viongozi Afrika (African Women Leaders Network -AWLN), Ellen Sirleaf aliyewasili jioni ya 19 Aprili 2026.
Wawili hao ni miongoni mwa wajumbe watakaoshiriki Mkutano wa Kamati ya Uongozi ya AWLN.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Zewde amepokelewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa.
Katika ziara yao wawili hao pia watakutana na viongozi wa Serikali, Dini, Asasi za kiraia, vyama vya siasa na makundi ya wanawake,mkazo ukiwa umewekwa katika kuhamasisha wanawake na maendeleo jumuishi.



Comments
Post a Comment