MWENGE WA UHURU WATUA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA


                                          Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

    Mwenge wa Uhuru watua Mkoa Kaskazini Unguja ambako pamoja na mambo mengine utazindua uwanja wa michezo jumuishi, uliopo Jimbo la Kijini. 

                       

Taarifa ya Mwakilishi wa Kijini, Badria Attai Masoud  kupitia mitandao yake ya kijamii imesema kuwa pia Mwenge huo utakagua ujenzi barabara ya Kijini na mirad yenye mchango mkubwa kwa jamii.

Mwenge huo pia  utapita Wilaya ya Kaskazini 'B' kabla ya kumalizia Kaskazini 'A' 12 April 2026.

Mwakilishi Atai ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, anasema wana uenzi Mwenge kwa vitendo kwa kufanyakazi kwa bidii, kuilinda amani na kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo kwa mustakbari bora wa Taifa.



Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA