MWANG'ONDA ATAKA FIDIA NDANI YA SIKU TANO WANAOPISHA BARABARA HONDOGO

                                      Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, Wazo Michael Mwang'onda ameagiza ndani ya siku tano wakazi wa barabara inayojengwa kiwango cha lami ya Hondogo kwa Shija, Kibamba Manispaa ya Ubungo, wawe wamelipwa fidia zao ili ujenzi wa barabara hiyo muhimu kwa wananchi uweze kutekelezwa inavyotakiwa. 

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.6, Mwang'onda alisema anaridhishwa na maendeleo ya ujenzi lakini anasikia kuna watu hawajalipwa fidia zao ili kuruhusu mradi kuendelea

"Nawaagiza ndani ya siku tano wawe wamelipwa fidia zao ili barabara hiyo muhimu iweze kukamilika kwa wakati" alisema kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru.

Mara baada ya agizo hilo aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo ya Kwa Shija, Hondogo hadi Kibwegere kunapojengwa Chuò cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kisha inakutana na Barabara Kuu ya Kibamba, ambayo inaenda  kuungana na ya Mpiji hadi Barabara ya Bagamoyo.





1.


2.


3.








Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA