Na Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na wakazi wa majumba ya Mjerumani Kikwajuni kwa kufikia maridhiano ambayo sasa yanatoa nafasi ya kuanza utekelezaji wa mradi ujenzi wa nyumba bora za kisasa ambazo zinatarajiwa kubadili mandhari ya Mji wa Unguja. Akizungumza na wanahabari waliofika ofisini kwake, leo 05 Machi 2026, CCM Kisiwandui kujua kinachoendelea kwenye mradi huo kutokana na kujitokeza sintofahamu baina ya baadhi ya wakazi na serikali, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema kufuatia maridhiano hayo mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani Milioni 45 sasa unaenda kutekelezwa. Alisema tayari Tsh.Bilioni 1.8 zimelipwa kwa wananchi waliokuwa wakiishi katika nyumba zilizopo katika maghorofa hayo yaliy...
Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakitamvumilia mteule yeyote wa Rais wa Awamu ya Nane, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wala taasisi yoyote itakayoshindwa kusimamia utunzaji wa miundombinu ya kisasa inayojengwa Zanzibar kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Akitoa tathmini ya ziara inayoendelea ya Rais Dkt. Mwinyi ya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu wa Kamati Maalum NEC, Zanzibar Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema kote walipoenda katika ziara hiyo, Rais Dkt. Hussein Mwinyi anasisitiza utunzaji miundombinu. "CCM tunaunga mkono kauli yake na tunafuatilia na tunasisitiza kuwa hatutamvumilia mteule au mtendaji yeyote atakaye zembea kwenye eneo lake n...
WAZIRI wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ijipange ipasavyo kuhakikisha kuwa inachangia upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ambayo imeainisha kuwa na uwiano wa Pato la Taifa wa TSh.Trilioni 1 ifikapo mwaka 2050. Balozi Omar alisema hayo alipokutana na kuzungumza na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TRA wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mamlaka hiyo, ikiwa na mara yake ya kwanza Tangu ateuliwe na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huo hivi karibuni. Alisema kuwa Dira iliyomaliza muda wake iliitaka Tanzania kufikisha uwiano wa Pato la Taifa wa Dola za Marekani bilioni 90 hadi kufikia mwaka 2025 lakini makadirio mapya yanataka kiwango hicho kifikie dola za Marekani Trilioni 1 ambazo TRA inatakiwa kujipanga ipasavyo kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa kiwango cha asilimia 70 ili kutekeleza Dira hiyo ipasavyo. B...
Comments
Post a Comment