MBETO: VIONGOZI CHADEMA HAWANA HISANI WALA KUMBUKUMBU
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaja safu ya viongozi wapya wanaokiongoza Chadema kwa sasa, wengi kati yao ni wanaharakati 'Uchwara' na si wanasiasa kwa maana hawana sifa hiyo.
Kauli hiyo ya CCM, imefuatia kitendo kisicho cha kizalendo cha Chadema kuandikia barua Umoja wa Afrika (AU) kupinga uteuzi wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mjumbe Maalum katika Pembe ya Afrika.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Komredi Khamis Mbeto Khamis alisema kitendo hicho kimekitia aibu Chadema na kuonyesha utovu wa adabu walio nao.
Mwenezi huyo alisemasafu mpya ya Viongozi wa Chadema hawana shukrani wala kumbukumbu.
Mbeto alisema kama kuna Rais aliyekuwa madarakani, akabeba dhima ya kuheshimu utawala bora wa sheria, demokrasia na kuenzi haki za binadamu hajatokea kama Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete.
"Wakati Dkt. Kikwete akiwa madarakani , kulikuwa na uhuru mpana wa vvyombo vya hjabari, ustawi wa demokrasia shirikishi na watu wameweza kukosoa kadri watakavyo" alisema Mwenezi Mbeto.
Alisema viongozi wa Chadema wameingia Ikulu na kufanya majadiliano ya kiTaifa wakati Dkt. Kikwete akiwa Rais hivyo Isingetegemewa viongozi wa Chadema watamke maneno yasio na Afya wala mantiki.
Katibu huyo Mwenezi alisema baadhi ya wana CCM, walimkabili Rais Kikwete, wakimtaka asiwakaribishe Chadema Ikulu kwani wanapotoka hupanda majukwaani na kumtukana bila sababu zozote.
"Utawala wa Rais Kikwete ulipofungua milango ya demokrasia, utawala bora, uvumilivu wa kisiasa na kuanza kusomwa Ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hadharani" alieleza.
Mbeto alisema, hatua ya Chadema hadi kufikia kuuandikia barua Umoja wa Afrika wakitaka kupinga uteuzi wa Dkt. Kikwete ni zaidi ya upuuzi uliopitiliza.
"Dunia imeushuhudia Utawala wa Dkt. Kikwete ulivyoheshimu haki, demokrasia na mijadala ya Bunge kuonyeshwa mubashara kupitia runinga . Wabunge wa Chadema ndio waliompigia makofi Dkt. Kikwete alipongia Bungeni baada ya kustaafu kwake Urais" alieleza Mbeto.
Hata hivyo Mwenezi huyo alisema sifa za Dkt. Kikwete Kitaifa, Kikanda na Kimataifa, utumishi na uwajibikaji wa Serikali yake umevunja rekodi.
Dkt. Kikwete akiwa Ikulu, alisema Mbeto, aliwaalika viongozi kadhaa kuitembelea Tanzania
"Marais kama Jim Tao, Xi Jinping wa China, Barack Obama na Wastaafu wawili wa Marakani G. W. Bush na Bill Clinton waliitembelea Tanzania.Kuona na kujua yote haya hakuhitaji tochi wala kufikia elimu ya juu.

Comments
Post a Comment