MBETO - SINA MASHAKA NA DEMOKRASIA YA TANZANIA

                                       Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

KATIBU wa Kamati Maalum NEC Zanzibar  Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Komredi Khamis Mbeto Khamis anasema hana mashaka na hali ya kidemkrasia iliyopo nchini kwani zaidi ya nchi zingine zikiwemo zinazojinasibu kupevuka kidemokrasia ikiwemo Marekani.

Mbeto akizungumza katika mdahalo wa Miaka 62 ya Muungano uliofanyika Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Mjini Unguja, 25 Aprili 2026, alisema kuwa hivi sasa watu wanakosoa hadi masuala ya usalama wa Taifa hadharani hadi kwenye mitandao ya jamii.

Alisema hata huko Marekani mtu hawezi kukosoa vyombo vya ulinzi na usalama kama inavyofanyika huku hiyo ni wazi kuna uhuru mpana wa watu kutoa mawazo yao.

"Demokrasia ya Tanzania ni pana sana, leo kuna watu wanatukana viongozi, huwezi kukuta nchi nyingine " anasema Mbeto.

Anabainisha kuwa demokrasia pana inayotoa uhuru wa watu kutoa mawazo yao isitumike vibaya na watu watambue kuwa licha ya demokrasia pia kuna sheria, hivyo ni vema kutambua kuwa viongozi waliopo madarakani ni kwa mujibu wa sheria.

Komredi Mbeto alisema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaamini katika ushirikino na maridhiano na ndio maana ya falsafa ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan.

"Tunaweza kuitumia vizuri hiyo falsafa na ndio maana akipokea ripoti ya Tume ya Jaji Chande kasema ataunda tume ya maridhiano na pia mchakato wa Katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu ujao 2030 alipokuwa azindua kampeni za CCM za uchaguzi mkuu 2025 Kawe, Jijini Dar es Salaam.

Alisema suala la Muungano ni muhimu kwa usalama wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

"Kuna kitu kwa kiingereza kinaitwa given take kwa maana katika Muungano kuna vitu unapata, kuna unavyopoteza mkazo ni maslahi ya Taifa" alisema.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA