MBETO: MUUNGANO TANGANYIKA, ZANZIBAR NI AZIMIO LA ACCRA 1958

             

                                            Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

CHIMBUKO la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar linatajwa kuwa ni azimio la mkutano wa wapigania Uhuru wa nchi za Afrika, waliokutana Accra, nchini Ghana 1958, Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume akiwa mmoja wao.

Azimio hilo lilifikiwa katika mkutano wa viongozi wapigania uhuru wa Afrika walipokutana nchini humo mwenyeji wao akiwa Rais wa Ghana wakati huo, Kwame Nkrumah.

Katika mkutano huo, anasema Komredi Mbeto moja ya maazimio ya nchi za Afrika ilikuwa kuendelea kupigania uhuru na ukipatikana waungane.

“Miezi mitatu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Karume akaanza, akamwambia Mzee Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tuungane akiakisi azimio la Accra” anasema Mbeto.

Pia Muungano na Tanganyika upande mwingine Hayati Karume aliutaka ili kuimarisha umoja na kuzidi kuimarisha ulinzi na usalama wa Zanzibar.

Kipindi hicho cha baada ya mapinduzi ya wananchi yaliyoratibiwa na vijana wa Afro Shiraz Party na kuung’oa utawala wa kisultani, kulikuwa bado 

kuna viashiria vya watu kutaka kupindua hali ambayo ilionwa kitambo na wapigania uhuru hao na kuwa na azimio la Accra kuitaka nchi za Afrika zinazopata uhuru kuungana ili kuweza kujiimarisha kiulinzi na kiusalama.

Mwenezi huyo akiuelezea zaidi dhana ya mapinduzi, anasema uzoefu unaonyesha siku zote yanapofanikiwa popote Duniani huwa yameungwa mkono na wananchi na ndivyo yalivyokuwa ya Zanzibar.

“Hayati Karume kutokana na kuwa mtu wa watu, mara nyingi alikuwa akitoka Ikulu na kwenda zilipokuwa Ofisi za Afro Shiraz (sasa Ofisi Kuu CCM Kisiwandui) ambako aliwasikiliza wananchi na kucheza Dhumna na wenzake”anasema Mbeto.

Anabainisha huo ndio ulikuwa utaratibu wake hadi ilipofika 07 Aprili 1972 majira ya jioni, watu wanaodaiwa wapinga maendeleo na umoja wa waZanzibari, wakamuua Rais Abeid Amani Karume ambaye leo 07 Aprili 2026 ni kumbukizi ya miaka 54 toka kifo chake.

Mbeto anabainisha kuwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, kumbukumbu zipo za matundu ya risasi zilizomuua Hayati Karume na kuwajeruhi wenzake, picha na majina ya waliokuwa wakicheza nae dhumna na ana enziwa kutokana kama Rais pekee aliyeleta mapinduzi ya maendeleo Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), chini ya Rais Dkt. Hussein Mwinyi inatimiliza kwa vitendo yote ambayo Hayati Karume aliyataka kwa wananchi wake ikiwemo makazi bora na ya kisasa, huduma za afya na elimu bila malipo kwa waZanzibari wote.

Mwenezi huyo anasema pamoja na mambo mengine, Hayati Rais Karume ambaye awali alikuwa kuli wa kubeba mizigo bandarini na baadae kuwa baharia na kusafiri takribani nchi zote ulimwenguni, alikuwa ni kiongozi wa namna yake Afrika.

“Walio wengi wanamtaja Rais huyo wakimhusisha na Mapinduzi na Muungano pekee lakini amefanya mambo mengi kupitia jumuia za kijamii kabla na baada ya mapinduzi katyika sekta takribani zote ikiwemo michezo” anasema Komredi Mbeto.

 

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA