MBETO: KUNA HOMBWE LA VIJANA KUTAKA UONGOZI, KUITWA WAHESHIMIWA

                                          Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

VIJANA wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wameshauri wasome na kuijua vizuri historia ya nchi na ya waasisi wa Taifa lao na sio kukimbilia uongozi na kutaka kuitwa ‘Waheshimiwa’ ili hali kuna vitu hawavijui.

Akizungumza katika mahojiano maalum Ofisi Kuu CCM Kisiwandui, Mjini Unguja, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo Komredi Khamis Mbeto Khamis alisema ni vema vijana wakaujua uongozi kabla hawajautaka.

Alisema kila kijana anataka aitwe mheshimiwa nae binafsi anapenda vijana washike uongozi kwani baada ya kuondoka wazee katika uongozi nani watashika nafasi zao lakini wanatosha?.

“Wazee kina karume wameondoka, je hatuwezi kuwa na Karume mwingine?” alihoji Mbeto na kuongeza kuwa ni lazima wasome kwa utashi wao waujue uongozi” alisema Mwenezi huyo.


Alibainisha kuwa ni lazima wajue nidhamu ya uongozi, wasome historia ya nchi yao na ya waasisi wa Taifa lao na katika kusoma watapata maarifa ya kujua ulimwengu unaendaje. 


“Niwaombe vijana wasome sana, wasome historia yao, wasome ulimwengu unaendaje, wasome uongozi, nidhamu ya uongozi ikoje na kikubwa wasiwe waoga” alisema.


Alisema vijana wanatakiwa wanyooke kwenye misimamo yao na nyeupe waseme nyeupe, nyeusi waseme nyeusi na jambo hilo kuna ambao litawachukiza lakini historia itaandikwa.


Komredi Mbeto ambaye anaamini pia kuwa uongozi ni kipawa kutoka kwa Mungu anatanabaisha kuwa maarifa hupatikana kwa kusoma vitabu vya wanafalsafa mbalimbali ili kujua dunia inaendaje.


“Leo unamwalika kiongozi unamuambia ataje historia ya nchi yake au viongozi wa Taifa anaanza kutafuta maneno, anahangaika” alisema Mbeto.


Anabainisha kuwa kijana kutambua historia ya Taifa lake lilipotoka, lilipo na linapoenda ndio jambo linalojenga uzalendo.


Mwenezi huyo ambaye amepata kufanyakazi na marais takribani wote isipokuwa Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere wakiwa wajumbe wa NEC, anasema viongozi hao wote kaulimbiu yao ilikuwa nchi, uzalendo kwanza.


Mbeto anawahimiza vijana wachape kazi  inapotokea wakapewa dhamana na waache kujipendekeza kwa viongozi na kuwafitinisha na kuwaumiza wenzao.


Alibaisha kuwa kijana unapopewa dhamana chapa kazi kwani utendaji huwa haujifichi hivyo hata ukifanyiwa fitina ya namna gani kazi zako zitakulinda.


Alisema kipindi hiki ambacho CCM inaekea kwenye chaguzi za ndani ya chama na hata zingine, vijana wanapaswa kuwaangalia waliowazunguka hao wanaotaka uongozi.

Anasema hali za watu walivyo itawasaidia kumjua huyo mtu ni wa namna gani.


“Unakuta mtu miaka 30 yupo kwenye uongozi lakini waliomzunguka hali zao zipo vile vile, mtu huyo hafai ina maana ni mbinafsi” anasema Mbeto.


Anasema na kuongeza kuwa uongozi ni kuacha alama kama alivyofanya Rais Karume na sasa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt, Hussein Ali Mwinyi anatekeleza kwa vitendo tena kwa wakati.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA