MBETO: DKT. MWINYI ANAPITA KATIKA MAONO YA HAYATI KARUME
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi anapita katika maono ya Rais wa Kwanza, Abeid Amani Karume katika kuwaletea watu wake maendeleo.
Akizungumza Mjini Unguja leo 11 April 2026, Katibu wa Kamati Maalum, NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo, Komredi Khamis Mbeto Khamis alisema kuwa Hayati Abeid Aman Karume aliwajali waZanzibari ndio maana alihakikisha wote wanapata makazi bora, pia alihakikisha huduma bora za afya, elimu, miundombinu ya barabara na huduma za kijamii.
"Nawaomba vijana wajifunze historia ya nchi yao ili kujua walipotoka, walipo na wanapokwenda" alisema Komredi Mbeto na kuongeza kuwa utulivu, amani na mshikamano ndio tunu ambayo waasisi wa Taifa waliihimiza.
Mwenezi Mbeto alibainisha kuwa Hayati Rais Karume alijenga miundombinu ya barabara ambazo leo zinaitwa pana kwa kuwa hazikuwepo.
"Rais Dkt. Mwinyi ndio anayoyafanya, kajenga kilometa 1000.9 za barabara za lami za juu (Fly Over) na za chini" alisema Mbeto.
Aidha mwaka1960 hayati Karume aliweka jiwe la msingi ujenzj nyumba za maendeleo na kwa kufuata maono yake leo Dkt. Mwinyi hivi sasa anajenga nyumba bora za makazi ya wananchi Unguja na Pemba.
Komredi Mbeto anazitaja nchi nne za kwanza kuyatambua Mapinduzi ya Zanzibar kuwa ni Urusi, China Ujerumani Mashariki na Cuba.
"Ujerumani Mashariki walitupa msaada wa kutujengea nyumba 158 zinaitwa za Mjerumani hadi sasa zipo na kumuenzi Karume tunazivunja na kujenga nyingine mpya za kisasa zaidi ya 1000" alisema na kuongeza kuwa lengo la yote ni kuhakikisha wananchi wanaishi katika nyumba bora za kisasa.






Comments
Post a Comment