MAONYESHO WASICHANA KATIKA TEHAMA YAVUTIA WENGI DODOMA
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Switbert Zacharia Mkama ni miongoni mwa watu waliovutiwa na bunifu za wasichana katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), wakati alipotembelea mabanda ya wanafunzi Shule ya Awali hadi Elimu ya Juu, yaliyofanyika, Ukumbi wa Jiji, Dodoma.
Maonyesho hayo yamefanyika baada ya mafunzo waliyopata wanafunzi hao.
Naibu Waziri Mkama alitembelea ili kujionea bunifu na ujuzi wa TEHAMA walioupata kupitia mafunzo mbalimbali ambayo yalifanyika na kilele chake 23 Aprili 2026 ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA.




Comments
Post a Comment