MAMLAKA HIFADHI YA NGORONGORO YAJIANDAA AFCON 2027
Na Mwandishi Wetu, Arusha
KATIKA kujiandaa na ugeni mkubwa unaotarajiwa kuwepo nchini kwa utalii wakati wa Michuano ya Soka ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro (NCAA), leo 27 Aprili, 2026 imeanza kutoa mafunzo ya kimkakati kwa watumishi wake 32 kutoka idara mbalimbali ili kujiimarisha kiujuzi na kuboresha huduma kwa wateja.
_Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayesimamia Huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo._
Akifungua mafunzo hayo Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayesimamia huduma za utalii na Masoko Mariam Kobelo, alisema lengo la mafunzo ya huduma kwa wateja ni kuhakikisha kila mtumishi ana jicho la utalii kuhakikisha mtalii akifika Ngorongoro anahudumiwa kwa viwango vya kimataifa.
_Mmoja kati ya wataalam kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), akitoa mada wakati wa mafunzo hayo._
“Mwaka 2027 tutakuwa na AFCON, Ngorongoro tumeanza kujipanga kwa kuhakikisha kila huduma tunayotoa kwa wageni inakuwa na viwango vya kimataifa na kuhakikisha tunatumia fursa ya mashindano hayo kupokea watalii wengi na kuwahudumia vizuri ili wanaporudi kwao waendelee kuwa mabalozi wa kuitangaza Tanzania” alisema Kamishna, Mariam.
_Washiriki, wakufunzi na mgeni rasmi wakiwa kàtika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo._
Mafunzo hayo ya siku mbili yanaendeshwa na wataalam kutoka Chuo cha Taifa cha utalii chini ya uratibu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.




Comments
Post a Comment