KLINIKI TEMBEZI WAGONJWA WA SARATANI HADI VIJIJINI


                                             Na Atley Kuni, WAF-DODOMA

WAZIRI wa Afya, Mohamed Mchengerwa (Mb.) amezindua gari maalumu la Kliniki tembezi ya Magonjwa ya Saratani kwa Wanawake kwenye Hospitali ya Kanda Benjamin Mkapa (BMH) Jijini Dodoma huku shabaha ikiwa nikuwafIkia wakimama walio wengi vijijini.

Akizindua gari hilo, Waziri Mchengerwa amewataķa watumishi wa Afya kote nchini kuendelea kufanya kazi kwa bidii, moyo wa kujitoa na maaarifa ili waTanzania wapate huduma zenye tija.

"Jiepusheni na vitendo viovu vinavyoweza kuichafua BMH na Serikali kwa ujumla kama vitendo vya rushwa, toeni huduma bora kwa mteja, lugha nzuri, mkurugenzi mtendaji endelea kuwakumbusha watumishi kila wakati juu ya Wajibu wao,  vikao vya kukumbushana majukumu na wajibu wa watumishi wote vifanyike" amesisitiza, Mchengerwa

Ametaka watamushi wa BMH kutambua kuwa wana wajibu wa kufanya kazi asubuhi, mchana na usiku ili matokeo yaonekane ambayo yatasaidia na kuwashawishi watoa maamuzi kwenye mchakato wa kuipa hadhi BMH kuwa Hospitali ya Taifa.

Akiongea katika hafla hiyo, Mratibu Mkazi wa Mradi Mtambuka wa Saratani za wanawake Afrika Mashariki, Dkt. Sara Maongezi amesema kuwa, mradi huo ni wa miaka minne, kuanzia 2025 huku ukilenga kupunguza madhara yatokanayo na saratani kwa wanawake ikiwemo kuboresha vituo vya saratani na kugawa vifaa vya matibabu ya saratani ikiwemo kliniki hiyo tembezi yenye thamani ya TSh.Mil. 272. 

"Kliniki tembezi tunayoitoa ni kwa ajili ya kuwezesha uchunguzi wa saratani ya shingo ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti kwenye maeneo ya vijijini ambapo  wakina mama wengi hawawezi kufika Hospitali kwa urahisi katika zinazotoa huduma hizo amesisitiza Dkt. Maongezi.


Awali akimkaribisha Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Prof. Abel Makubi amesema kuwa mradi huo ni muendelezo wa makubaliano ya ushirikiano (MOU) ambao tulisaini na Taasisi ya Afya ya Aga Khan mwaka 2025 kwenye maeneo ya mafunzo, utafiti na matibabu na mradi utasaidia kuhudumia wananchi takribani Milioni 14 wa mikoa ya Dodoma na inayozunguka Kanda ya Kati kwa ujumla.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA