HUDUMA ZA AFYA SEKTA BINAFSI ZAJADILIWA DODOM
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
NAIBU Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, leo Aprili 20, 2026 amewasili katika Ukumbi wa Jiji uliopo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kushiriki Mkutano wa Wadau wa Sekta Binafsi ya Afya.
Naibu Waziri Dkt. Samizi ambaye amepokelewa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe, anamwakilisha Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa.
Mkutano huo umebeba kauli mbiu isemayo, “Kuimarisha Ubora na Ufanisi katika Utoaji wa Huduma za Afya za Sekta Binafsi kuelekea Upatikanaji wa Huduma za Afya kwa Wote nchini Tanzania".
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili nafasi ya sekta binafsi katika kuboresha huduma za afya na kufanikisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi wote.

.jpg)

Comments
Post a Comment