BARABARA KM 9.3 MKWAJUNI-KIJINI KUKAMILIKA JUNI 2025


                                        Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

BARABARA ya Mkwajuni hadi Kijini yenye urefu wa Kilometa 9.3 inatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu 2025 hivyo kurahisisha usafiri na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wote.

Akizungumza mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuhitimisha mbio zake Wilaya ya Kaskazini 'B',  11 April 2025, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Badriya Atai Masoud alisema ujenzi wa barabara hiyo unaendelea vizuri na anaamini kuwa utakamilika kwa wakati.

Naibu waziri huyo ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kijini kwa tiketi ya CCM, alisema licha ya barabara hiyo pia Mwenge uliangazia kuwekwa jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa michezo wa kisasa katika jimbo hilo.

Alisema uwanja huo wa wilaya wenye hadhi ya Mkoa, unaonyesha dhamira ya dhati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi ya kuendeleza vipaji vya vijana na kukuza sekta ya michezo.

"Pongezi sana Rais Dkt. Samia na Rais Dkt. Mwinyi kwa uongozi mahiri, thabiti na wenye maono ambao unaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na zenye tija' alisema Naibu Waziri Badriya.

Kuhusiana na Mwenge wa Uhuru alisema umekuwa taa ya matumaini na wao kama wasaidizi wa viongozi wakuu wa kiTaifa wanaahidi kuendeleza juhudi hizo kwa vitendo ili kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa ubora na kuwanufaisha wananchi waliowapa dhamana ya kuwatumikia.



Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA