WANANCHI WATAKIWA KUIOMBEA DUA NCHI AMANI IDUMU
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema nchi ipo katika amani baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu na kuwahimiza wananchi kuendelea kuiombea dua.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo jana, tarehe 15 Machi 2026, alipojumuika na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika futari ya pamoja aliyowaandalia.
Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu, Mkoa wa Mjini Magharibi, na kuhudhuriwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi. Pia imehudhuriwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewashukuru wote walioshiriki katika futari hiyo na kuwatakia heri katika kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Magharibi, Talib Ali Talib, amemshukuru Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa kuwaandalia futari hiyo aliyoielezea kuwa ni kielelezo cha imani na upendo kwa wananchi anaowaongoza.
Futari hiyo imehudhiriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, viongozi mbalimbali wa Serikali na Dini.







Comments
Post a Comment