SIKU 100 ZA DKT. MWINYI SEKTA ELIMU


                                         Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

WAKATI anaingia madarakani 2020 kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Hussein Ali Mwinyi 2020, anasema kipaumbele cha kwanza cha serikali yake ni elimu.

Anasema, tunatambua elimu ndio itamuwezesha kila mmoja wetu kuweza kujikomboa, kuondokana na umaskini unaotukabili.


Anaongeza Bajeti ya Elimu kutoka Tsh.Bilioni kutoka Bil. 265 mwaka 2021 hadi 457 ongezeko la asilimia 72 lengo kuongeza juhudi katika suala zima la elimu.
 
Anawaambia Wizara ya Elimu lijengwe jengo la shule la mfano, kisha liangaliwe kama litafaa na shule ya msingi Fuoni inafanywa ya majaribio.
Shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 3,000 ina madarasa 23 hivyo na kufanya wanafunzi kusoma kwa zamu mbili hadi tatu kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi.


Siku ya uzinduzi wa shule hiyo miaka miwili iliyopita, Rais Dkt, Mwinyi anakuwa mgeni rasmi na anasema niliwaambia tujenge jengo hapa Fuoni, tuangalie kama linatufaa.
 
“Ndio maana nipo mwenyewe leo nimekuja hapa kutazama hiki kitu kinafanana na ninachokitaka? Nimeridhika hiki kitu kizuri, kimejengwa kwa muda mfupi” anasema wakati wa uzinduzi huo.


Anabainisha kuwa kama ungekuwa ujenzi uliozoeleka wa matofali ya kawaida, pangejengwa hata kwa miaka miwili.

Rais Dkt Mwinyi baada ya kuikagua, anasema ameridhika, ina viwango na inawafaa na si kwa ajili madarasa bali pia maabara na chumba chenye kompyuta za kisasa.

“Maabara ya kisasa kabisa, mie sikujua kama hata shule za msingi zina maabara ndio naona leo humu ndani ni ya kisasa kabisa” anasema.


Anabainisha kuwa aliwaambia wajenzi, kama watawajengea shule moja ya mfano wakaridhika nayo. Wapo tayari kuingia nao mkataba wajenge zingine kama hizo 20, Unguja na Pemba.

Anasema vinatakiwa vitu vinavyokwenda na wakati kama hivyo na anatanabaisha kuwa wanafunzi wakianza kujifunza kompyuta mapema, watakwenda na kasi ya dunia inavyotaka.


Toka wakati huo hadi hivi sasa zinapozungumziwa siku 100 za Dkt. Hussein Ali Mwinyi madarakani, jumla ya shule mpya 60 zimejengwa kati ya hizo 23 za ghorofa, Unguja na Pemba.

Sanjari na hilo kunako 21 Mei 2025, mkataba wa mkopo wenye thamani ya TSh.240 bilioni umesainiwa Ikulu Zanzibar baina ya SMZ na Benki ya CRDB kwa ajili ya ujenzi wa shule 23 za msingi na sekondari za ghorofa, Zanzibar.


Pia shule 20 zipo katika majaribio  ya   matumizi ya mfumo wa Tehama katika ufundishaji kila darasa likiwa na ubao janja ‘Smart board’ na mwalimu anaweza kufundisha zaidi  ya darasa moja akiwa ofisini kwake huku akiona kila kinachoendelea darasani.

Katika kipindi kifupi mengi yameonekana ndani ya siku hizo na mengi yamefanyika na si kwa maneno bali vitendo kwa juhudi na juhudi kubwa ikielekezwa katika ujenzi wa miundombinu.

Shule za kisasa za ghorofa, ukarabati wa madarasa na maabara zimewezesha mazingira bora kwa wanafunzi na kuongeza kiwango cha ufaulu na kuondoa msongamano na kufanya maeneo mengi kuwa mkondo mmoja badala ya mwili hadi mitatu.



“Tunashukuru sana Dkt. Mwinyi katujengea ‘skuli’ (Shule), skuli ambayo ina miundombinu mizuri kwa wanafunzi, ikiwemo madarasa ya kompyuta, Library (maktaba) na maabara pia nzuri” anasema Mwanaisha Vuai Ameir, mwanafunzi shule ya sekondari Kiwani.
 
Ndani ya kipindi cha siku hizo 100 za Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, zaidi ya walimu 5,265 wameajiriwa, kompyuta za kisasa 3,000 serikali imezigawa kwa shule za msingi na sekondari na vitabu milioni 1.3 vimechapishwa.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA