MWAKILISHI ATAKA USHIRIKIANO KUTATUA CHANGAMOTO KIJINI


                                     Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MWAKILISHI Jimbo la Kijini,, Mkoa wa Mjini Magharibi Badriya Atai Masoud ametaka jamii kushirikiana ili kuhakikisha katika maeneo yao wanapata huduma bora na miundombinu inayokidhi mahitaji halisi ya wananchi.

                       

Akizunguumza wakati wa ziara yake jimboni kukagua maendeleo ya jamii pamoja na dini, Mwakilishi huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi alisema kuwa ni wajibu wanajamii kushikana mikono.

Mwakilishi huyo katika kukabiliana na changamoto tofauti zinazowakabili wapiga kura wake na kusukuma mbele maendeleo ya jamii na dini, alikabidhi mabati kwa ajili ya kuezekea msikiti unaojengwa eneo hilo ili kuweka mazingira bora ya kiswalia na pesa kwa ajili ya ujenzi wa mashimo ya vyoo vya madrasa katika msikiti huo.

Pia Mwakilishi Badriya alisema amejitolea ujenzi wa mashimo hayo ili kuhakikisha wanasoma katika mazingira salama yenye stara ma yanayozingatia afya bora.

Pia Makilishi  huyo alifanya vipimo vya mazuria katika msikiti huo mpya unaojengwa.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA