MBETO: MAGUFULI, RAIS SAMIA, RAIS MWINYI MADAKTARI KAZI NA UTU


                                         Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

KATIKA hitimisho la maadhimisho ya miaka mitano toka afariki Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya   Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis anabainisha kuwa kauli mbiu yake "Hapa Kazi tu" ambayo ndani yake ina utu ina enziwa vilivyo na aliowaacha.

Mbeto alisema kuwa pamoja na misimamo na majukumu mazito aliyokuwa nayo Dkt. John Pombe Magufuli lakini pia alikuwa na utu na aliwasaidia na kuwasikiliza watu wa kada zote kama afanyavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. Samia na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

"Kuna clip ipo mitandaoni aliyekuwa Rais, John Magufuli akilia baada ya kuguswa na hali ya mama mjane kama sikosei, aliyeenda kumuona katika moja ya ziara zake" alisema Mbeto.

Alisema si jambo la kawaida Rais kulia na kutoa machozi hali inayoonyesha kuwa ana utu uliopitiliza.

"Ndio maana kifo  chake watu wote walilia" alisema Mwenezi Mbeto na kuongeza kuwa lilikuwa jambo la kawaida kusimamisha msafara na kuzungumza na wananchi wa kawaida.

"Mama Rais Samia kaja na 'Kazi na Utu, tunasonga mbele', kiasili yeye ni mpole na anafanya mambo mengi kwa jamii na wengi amewasaidia, kuna watu wanajua kuwa kama sio yeye hawajui wangekuwa wapi" alisema na kuongeza kuwa amejaa umama na huruma nyingi.

Alisema kipindi hiki cha Kwaresma na Ramadhan anafuturisha nchi nzima kupitia wakuu wa mikoa achilia mbali fedha anazotoa kusaidia misikitl na makanisa.

Mbeto alimtaja Rais Dkt. Mwinyi kupitiliza kwenye kazi na utu huku akitoa ushuhuda wa Rais Mwinyi kukubali mwaliko wa kufuturu nyumbani kwa mwananchi wa kawaida ambaye hana wadhifa wowote katika chama wala serikali.

"Juzi hapa kaenda kufuturu kwa Bwana Salum Maridhia, mtu wa kawaida na hayupo kwenye chama wala serikali, Misiba mingi anaenda, mingine ya wananchi wa kawaida kabisa" alisema na kuongeza kuwa, pia anatoa misaada mingi na mingine bila kutangaza.

Komredi Mbeto anasema kuna siku Rais Dkt. Mwinyi aliswali msikiti anaoutumia yeye Mbeto mara kwa mara na alishangaa mwisho wa Ibada viongozi wanasimama anakopota na kumshukuru kwa kuwafungia viyoyozi msikitini.

Mbeto alisema alikuwa hajui jambo hilo na hakuwa amelisikia kabla ya hapo hali inayoonyesha jinsi gari Taifa limejaaliwa viongozi wenye maono, bidii ya kazi na utu.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA