MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AGAWA FUTARI KIWANI
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amegawa futari kwa familia zaidi ya 1,156 za Sheia ya Kendwa katika hafla ya ugawaji iliyofanyika katika viwanja vya Mauwani, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa pili wa Rais ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani ametoa futari hiyo ambayo ni vyakula vya aina mbalimbali ili kuwasaidia wakazi hao kupata wepesi wa kujumuika na waislamu wengine katika funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Pia Makamu huyo wa pili alipata fursa ya kujumuika kwenye futari nyumbani kwake na viongozi mbalimbali, watoto yatima na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo la Kiwani.




Comments
Post a Comment