IDARA MAAFA NA DHARULA WAPO TANGA

Na Andrea Kadege, WAF-Korogwe

Viongozi kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Maafa na Dharura, wakiwa wameambatana na wadau wengine kutoka Taasisi za Serikali na binafsi wamemtembelea Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Zahara Msangi, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikao kazi cha tathmini ya matukio na athari za kiafya mkoani Tanga.

Ziara hiyo imelenga umuhimu wa kuwa na mfumo madhubuti wa utayari na mwitikio wa haraka dhidi ya majanga na milipuko ya magonjwa. 



Kupitia kikao kazi hicho, wadau watajadili takwimu za matukio yaliyotokea, kubaini mianya ya kiutendaji na kuweka mikakati shirikishi ya kuzuia, kugundua mapema na kukabiliana na athari za kiafya kabla hazijaathiri kwa kiwango kikubwa jamii.


Bi. Zahara ameipongeza Wizara kwa hatua hiyo ya kimkakati, akieleza kuwa tathmini hiyo itaimarisha kinga ngazi ya jamii, kuongeza uelewa wa vihatarishi na kuunganisha nguvu za sekta mbalimbali katika kulinda afya za wananchi.

Hatua hiyo inaakisi dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kila mkoa unakuwa na mpango kazi unaotekelezeka wa kukinga, kujiandaa na kukabiliana na dharura za kiafya kwa ufanisi na weledi zaidi.



Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA