DKT. MWINYI: IFTAR KITAIFA JUKWAA LILILO UNGANISHA WAISLAM ZANZIBAR


                                          Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa imendikwa historia ya kipekee kwa kubwa la Futari ya kiTaifa kwa mara ya kwanza lililowakusanya maelfu ya Waumini wa Dini ya Kiislamu katika kusanyiko la pamoja. tukio.

Akizungumza wakati wa futari hiyo 07 Machi 2026 katika Uwanja wa Neww Amaan Complex, Mkoa wa Mjini Magharibi, Rais Dkt. Mwinyi alisema tukio hilo ni jambo jema lenye thawabu kubwa mbele za Mwenyezi Mungu sanjari na kuwa jukwaa muhimu la kuwaunganisha Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na wananchi kwa ujumla katika kuimarisha mshikamano miongoni mwa wananchi.

Dkt. Mwinyi amewatakia waumini kuendelea kuzidisha ibada na dua na matendo mema katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku wakiendelea kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuijalia nchi amani, utulivu na mshikamano miongoni mwa wananchi wake.

Katika futari hiyo ambayo iliandaliwa na Ofisi ya Mufti Mkuu, Kamisheni ya Utalii na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Naibu Mufti, Sheikh Mahmood Mussa Wadi alisema tukio hilo ni muhimu na linaloongeza upendo miongoni mwa waumini.

Huku likichangia kuondoa chuki na kuimarisha mshikamano makundi mbalimbali ya  waumini wa dini ya kiislamu” alisema Naibu Mufti.


Comments