WAZIRI KAIRUKI: TANZANIA IPO TAYARI KWA AKILI UNDE


                                            Na Mwandishi Wetu, India

TANZANIA ipo tayari kushirikiana kuhakikisha matumizi ya Akili Unde nchini yanakuwa endelevu, imara na yenye ubunifu yakizingatia uimarishaji wa mazingira na matumizi ya nishati bora.

Akiwasilisha ripoti ya Tanzania katika mkutano Mkuu wa Masuala ya Akili Unde unaofanyika nchini India 18 Februari 2026, ikiwasilishwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki alisema, moja ya vipaumbele ni kuwekeza kwa kujenga vituo vya kuhifadhi Data.

Waziri Kairuki ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Jijini Dar es Salaam, alisema serikali inaimarisha ushirikiano na sekta binafsi wakiwemo watafiti, wabunifu na kuhakikisha matumizi ya Akili Unde yanaleta tija nchini.


Pembeni ya mkutano huo watalaam kutoka Tanzania wameshiriki katika vikaokazi vya mkutano huo kujadili jinsi ambavyo nchi itahakikisha matumizi ya Akili Unde yanakuwa jumuishi na endelevu.

Awali Waziri Kairuki alikutana na mawaziri kutoka nchi mbalimbali na kujadiliana na wawekezaji na makampuni makubwa yanayo ongoza kwa matumizi ya Aki.i Unde ili kuona Tanzania inanufaika vipi kupitia fursa mbalimbali za wadau.







 

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA