WAZAZI CCM WAKUMBUSHWA WAJIBU WA MALEZI
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa Kibamba na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki amewakumbusha wazazi kuendelea kuwa walezi bora kwa vijana.
Kairuki ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Ubungo alisisitiza kuwa ni muhimu kwa wazazi kukaa na kuzungumza na vijana wao, kuwalea katika kimaadili mema na kuwaandaa kuwa viongozi bora wa kesho.
Mbunge huyo alisema kuwa ameshiriki baraza hilo ili kutoa shukrani kutokana na mchango wa mkubwa katika kukipambania Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu uliopita 29 Oktoba 2025.
Aliwapongeza kwa ushindi mkubwa wa asilimia 97 waliompatia Dkt. Samia Suluhu Hassan na pia alipokea ombi la changamoto ya ujenzi wa nyumba ya ya mtumishi wa jumuia hiyo (Katibu Wazazi Wilaya) na walimwambia kukosa makazi rasmi kunakwamishja utendaji kazi wa kila siku.
Mbunge Kairuki aliahidi kuchangia TShMiliioni 10 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba hiyo na pai aliahidi kuendelea kushirikiano nao katika kuiimarisha jumuia na kuwapongeza kwa uwekezaji wao wa kujenga Ofisi ya Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Ubungo.




Comments
Post a Comment