RAIS DKT. SAMIA AFUTURISHA TUNGUU, ZANZIBAR
Leo, 19 Februari 2026, nimejumuika na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, viongozi wa Siasa, Dini pamoja na wananchi katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.
Ninamshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kuandaa futari hii iliyotukutanisha pamoja katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Tukio hili limeendelea kuimarisha mshikamano, umoja na ushirikiano baina ya viongozi na wananchi, pamoja na kuonesha dhamira ya pamoja ya kuendeleza amani na maendeleo ya Taifa letu.
Ramadhani ni mwezi wa ibada, huruma na kujenga mahusiano mema.
Tuendelee kushikamana, kuheshimiana na kushirikiana kwa manufaa ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.




Comments
Post a Comment