RAIS DKT. MWINYI ASHIRIKI MAZIKO MAMA WA RC, UNGUJA


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi 23 Februari 2026, amejumuika na viongozi, wanafamilia na wananchi mbalimbali katika maziko ya mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,  Cassian Gallos Nyimbo, Theodosia Sylvester Mapunda yaliyofanyika katika Makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mama huyo wa Mkuu wa Mkoa, alifariki dunia tarehe 21 Februari 2026 na   Rais Dkt. Mwinyi ametoa pole akisema  anafanya kwa dhati Nyimbo, familia, ndugu na jamaa wote walioguswa na msiba huo.

"Katika nyakati kama hizi, mshikamano, upendo na faraja ni muhimu ili kuimarisha moyo wa subira na ustahimilivu" anasema katika salamu zake za pole na kueleza  kuwa anaungana na familia katika kumuombea Marehemu Theodosia Mapunda

 "Apumzike kwa amani, na Mwenyezi Mungu awajalie wanafamilia wake subira na faraja katika kipindi hiki cha maombolezo.


Hakika, Bwana ametoa na Bwana ametwaa; jina lake lihimidiwe" anasema Rais  Dkt. Mwinyi.



Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA