MBUNGE KAIRUKI AWAPA MATUMAINI SARANGA


                                     Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MBUNGE wa Kibamba, Angellah Jasmine Kairuki Mberwa ameahidi kushirikiana na mamlaka zingine kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa Kata ya Saranga, Kimara Jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Jimbo la Kibamba, Mbunge Kairuki alielezwa na wakazi   

wa Kata hiyo changamoto ya vivuko, watoto wa mtaa wa Upendo kutembea umbali mrefu kuifuata shule na changamoto ya miundombinu ya barabara.

Mbunge Kairuki alisema serikali inafanya jitihada mbali kukabili changamoto zinazowakabili na alikagua barabara ya Golani-Suka yenye kilomita 1.5 ambayo imechongwa na kuwekwa kifusi na pia ujenzi wa mita 200 wa barabara ya Kimara mwisho-King'ong'o kupitia ofisi za TRA inayojengwa kwa zege.

Kairuki alisema ni kusudio la serikali kuona wananchi wanapita katika barabara salama.

Aliwasifu na kuwashukuru wakazi waliojitolea kujenga baadhi ya vivuko na kuahidi kuwa anaunga mkono jitihada zao na atatoa sapoti kufanikisha vivuko vya kudumu.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA