MBUNGE KAIRUKI AGAWA VITIMWENDO KIBAMBA


                                           Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MBUNGE wa Jimbo la Kibamba ambaye pia ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki ametoa msaada wa vitimwendo 10 kwa wenye mahitaji maalum ili kuwawezesha kufanya shughuli zao za kila siku kwa urahisi zaidi.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi viti hivyo iliyofanyika, Ofisi za Mbunge Jijini Dar es Salaam 07 Februari 2026, Mbunge Kairuki alisema ataendelea kutoa msaada wa viti mwendo kwa wenye uhitaji maalum kwa utaratibu maalum ikizingatiwa kuwa mahitaji ni makubwa.




Kairuki alisema ataweka mfumo utakaohakikisha msaada huo unawafikia wenye uhitaji waliopo katika mitaa yote ya Jimbo la Kibamba.

Alisisitiza kuwa huo ni mwanzo tu wa jitihada zake za kuihudumia kundi hilo akibainisha kuwa watu wenye mahitaji maalum ni miongoni mwa makundi anayoyapa kipaumbele kikubwa.

Miongoni mwa waliopatiwa msaada huo ni pamoja ni pamoja na mwenyeulemavu aitwae Jackson ambaye licha ya hali yake hiyo ya ulemavu wa kutotembea, ameonyesha bidi kwa kuanzisha genge duka na huduma za uwakala wa kifedha.


Kutokana na hali yake na jitihada anazozionyesha katika kujiajiri, Mbunge Kairuki amemuongezea mtaji wa TShilingi 500,000 ili kukuza biashara zake na kuweza kujikimu zaidi kimaisha.

Wazazi na walezi wa wanufaika, wamemshukuru Mbunge Kairuki kwa moyo wake wa kujali na kuendelea kugusa maisha ya wenye mahitaji maalum. 



Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA