MBETO: WINGI WA BIDHAA KUSHUSHA BEI KWA WALAJI
Na Mwandishi Wetu, ZanzibarBAADHI ya bidhaa bei zipo juu katika masoko tofauti Unguja na Pemba katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na mahitaji kuwa makubwa na ukweli kuwa bidhaa hazijaanza kuingia kwa wingi toka Tanzania Bara hususan kipindi hiki cha 10 la kwanza.
Akizungumza 22 Februari 2026 mara baada ya kumaliza ziara ya kushtukiza aliyoifanya katika masoko na maduka mbalimbali, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo Cde: Khamis Mbeto Khàmis alisema bidhaa hazijaanza kuchanganya sokoni.
- Katika ziara hiyo mwenezi huyo alisema kuwa kilichobainika ni kuwa bidhaa bado hazijaingia zà kutosha hali inayofanya baadhi yake bei kuwa juu lakini anaamini kuwa kadiri siku zinavyokwenda zitaongezeka na bei zitakuwa rafiki kwa wananchi.
"Mwezi wenyewe ndio kwanza una siku nne, najua kwenye 10 la mwanzo huenda kukawa na changamoto kidogo kwenye bei lakini siku zinavyoenda nafuu itapatikana" alisema Mbeto.
Alitaja bidhaa kama Njugumawe, Mbaazi, Magimbi na Viazi Vikuu kuwa kwa sasa hazijaanza kuingia kwa wingi toka Tanzania Bara bei yake kidogo ipo juu na upande wa nafaka hakuna upungufu na bidhaa zote zipo sokoni na madukani.
Alìtaja bidhaa zinazotumika kwa wingi kipindi hiki za Sukari, mchele, Unga wa ngano na zingine kuwa hakuna upungufu zote zinapatikana na bei ni himilivu.
Kuhusu viungo hususan Iriki na nazi ambavyo kwa kiasi kikubwa vinatoka Tanga, Mafia na katika maeneo mashambani Unguja na Pemba bidhaa hizo zimeanza kuingia.
Mwenezi Mbeto ambaye chama chake CCM ndio kinaisimamia serikali katika kuwatumikia wananchi, amewaomba wafanyabiashara kupunguza bei za vyakula kipindi hiki cha Ramadhan.
"Nawaomba wajikite katika kuhudumia jamii, watoe Tahfif (nafuu) ili wananchi wanyonge waweze kumudu mahitaji yao ya kila siku" alisema na kuwataka wafanyebiashara na Mungu ili waweze kuchuma heri kesho kwani kipindi hiki wananchi wengi Unguja na Pemba wanakimbilia kwenye masoko kupataa mahitaji.
Awali Mwenezi huyo aliwatembelea wafanyabiashara wenye minada ya viungo na bidhaa za vyakula na kuwashajiisha kuagiza kwa wingi ili kumudu mahitaji ya wateja wao ili waweze kushiriki mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa amani na utulivu.
alizungumza pia na wafanyabiashara kwenye minada



Comments
Post a Comment