MBETO;: SIKU 100, MAMBO MAKUBWA ZANZIBAR
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ndani ya Siku 100 za utendaji wake amefanya mambo mengi makubwa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi zaidi ya 100 yenye thamani ya TSh.Trilioni 1.8.
Akizungumza Mjini Unguja leo 12 Februari 2026 kuhusiana na siku 100 toka Rais Dkt. Mwinyi awe madarakani, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema miradi hiyo 42 ipo Pemba na 68 Unguja na kimsingi ndani ya siku hizo 100 amefanya mambo makubwa na yapo wazi.
Mbeto alisema ni wazi kuwa kutokana na kasi yake asilimia 100 ya Ilani ataifikia kabla ya 2030.
Baadhi ya miradi Mwenezi Mbeto aliitaja kuwa ni pamoja na uzinduzi Kiwanda cha uzalishaji Vifaranga na chakula cha kuku, kuzinduliwa Soko kubwa la Kisasa la Mombasa sanjali na Kituo cha Afya Daraja la Pili, Tumbatu.
"Tumeshusha mabasi ya umeme 100 wakati wowote yataanza kutoa huduma, meli ya Mv Mapinduzi ipo katika majaribio ikisubiri kibari itoe huduma" alisema Mwenezi Mbeto.




Comments
Post a Comment