MBETO: RAMADHANI IWE KUCHUMA HERI SIO KIPATO
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
WAFANYABIASHARA Zanzibar wamekumbushwa kuweka nafuu ya bei kwenye bidhaa za vyakula ili kuwezesha walio wengi kumudu kupata futari na daku katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ulianza kutekelezwa nchini leo 19 Februari 2026.
Akizungumza na Mtandao wa HabariZenu, Mjini Unguja, Zanzibar, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kham8s Mbeto Khamis alisema kuwa huu ni mwezi wa kuchuma heri sio kipato.
"Niwaombe kwa niaba ya CCM kuutumia mwezi huu wa Ramadhan kufanya toba kwa Mwenyezi Mungu ambaye amekujaalia mwaka mzima hadi kufika sasa" alisema.
Mbeto pia amewaasa wale ambao Mungu amewabariki kipato kuwasaidia wale ambao hawana kwani ni mwezi mzuri wa kuweza kuficha shida za wenzetu na kuhakikisha wanatekeleza Ibada vizuri.
"Mwezi umekusanya mambo mengi, biashara ipo, ibada ipo pia ni mwezi wa kudumisha amani" alisema na kuwatakia waislam wote mfungo mwema wa Ramadhan.

Comments
Post a Comment