KAMISHENI YA UTALII YATOA MWONGOZO RAMADHANI ZANZIBAR


                                       Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

KAMISHENI ya Utalii Zanzibar imetoa mwongozo wa biashara ya utalii Zanzibar katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Taarifa hiyo ina wataarifu wadau wote wa utalii kuwa kipindi cha Ramadhani ni kitukufu kinachoathimishwa na jamii kubwa ya Waislam Zanzibar ambacho kinajumuisha kufunga, sala, tafakari.

Inabainisha taarifa hiyo, ikiwataka wadau kuheshimu thamani za dini na tamaduni ili kuhakikisha amani ya kijamii  na utalii vinaheshimu Ramadhani 2026 hivyo biashara zote za utalii, wauzaji na wageni kufuata miongozo ifuatayo.

Migahawa na maduka ya vyakula nje ya hoteli lazima ifungwe wakati wa mchana na kufunguliwa tena baada ya machweo (Iftar).

Huduma za chakula ndani ya hoteli na mashirika yanayofanana zinapaswa kutolewa kwa wageni tu waliokuwa kwenye hoteli na ndani ya majengo ya hoteli pekee. Kunywa, kula kuvuta sigara hadharani wakati wa mchana hairuhusiwi.Z

Vazi la heshima linahitajika kwenye maeneo ya umma na vazi la ufukweni au lenye kufichua mwili linapaswa  kubakia kwenye fukwe na maeneo ya hoteli pekee.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA