KAGERA WAZINDUA DAWATI LA UWEKEZAJI

                                                Na Mwandishi Wetu, Kagera

Zaidi ya wawekezaji na wafanyabiashara 100 wamehudhuria Kongamano la Uwekezaji pamoja na Uzinduzi wa Dawati la Uwekezaji lililofanyika leo tarehe 7/1/2026 katika ukumbi wa zamani wa Wilaya ya Bukoba Vijijini, mkoani Kagera.

Kongamano hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya uwekezaji na washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali , kueleza changamoto wanazokutana nazo, kujifunza na kujadili kwa kina masuala ya uwekezaji, vivutio vinavyotolewa na Serikali kupitia Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) pamoja na nafasi zilizopo mkoani Kagera.

Hafla hiyo ya uzinduzi na kongamano, limeandaliwa na TISEZA kwa kushirikiana na maafisa kutoka Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, likiwa na lengo la kusogeza huduma za uwekezaji karibu na wananchi na kutoa elimu ya uwekezaji kwa vitendo.

Kongamano hili na uzinduzi wa dawati la uwekezaji ni mojawapo ya hatua muhimu katika utekelezaji wa azma ya kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani, sambamba na kukuza uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA