DKT. ABBAS AONGOZA KIKAO MPANGOKAZI FOLUR
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi 21 February 2026 ameongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi wa Mradi wa Mifumo ya Chakula, Matumizi ya Ardhi, Maji na Urejeshaji wa Mandhari ya Misitu (FOLUR).
Kikao hicho pamoja na mambo mengine, kina lengo la kuimarisha usimamizi na uangalizi wa mradi pamoja na utekelezaji wa Mpango Kazi na Bajeti ya mwaka 2025/2026.
Kikao kimelenga kuangalia bajeti mpya na utekelezaji wake kikiwahusisha wadau wakuu ambao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Saleh Mohamed Juma, ambaye ni Mwenyekiti Mwenza pamoja na wadau mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.




Comments
Post a Comment