CCM: SHIKENI YA 'OMO' MAZUNGUMZO CCM, ACT YANAENDA VIZURI


                                        Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wanahabari na wananchi kwa ujumla kuisimamia kauli ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman 'OMO- aliyoitoa juzi 12 Februari 20226, katika mkutano alioufanya na viongozi wa chama hicho akiwa ziara ya kikazi Pemba kuwa mazungumzo ya kuelekea kuundwa Serikali ya Umoja wa kiTaifa   (SUK) Zanzibar yanaenda vizuri.

Akijibu swali kwa wanahabari kuhusiana na yalipofikia mazungumzo hayo kufuatia hatua ya ACT kusua sua kujiunga na serikali ya umoja wa kiTaifa kama takwa la Katiba ya Zanzibar linavyoelekeza, Mwenezi Mbeto alisema CCM inawasubiri kuunda serikali  hiyo ili kuwatumikia wananchi.

Alisema kuwa kulingana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita 2025 kutokana na ACT kushinda zaidi ya  asilimia 10 ya kura zote kama katiba inavyosema, ndio chama kinachoungana na CCM kuunda Serikali ya Umoja wa kiTaif kwa wingi wa kura na viti vya Uwakilishi, unawapatia mawaziri wanne na Makamu wa Kwanza wa Rais.

"Mpaka hivi sasa nafasi hizo wamekaimu maWaziri wa CCM tunawasubiri wao kwani zisingeweza kubaki tupu bila Waziri" alisema Mbeto.

Alibainisha kuwa suala la mazungumzo na hata wazo la kuwepo kwa SUK ni la CCM kufuatia Azimio la Butiama na liliamriwa kwenye vikao husika na likapitishwa kwa ajili ya utekelezaji.

Alisema baada ya kukubaliana Butiama lilipelekwa kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kisha Baraza la Wawakilishi na kura za maoni zilipigwa kuamua iwepo au isiwepo na mazungumzo yanayoendelea hivi sasa kuna mambo yanaweza kuzungumzika na kufanyiwa marekebisho lakini mengine ambayo ni ya kisheria na kikatiba yatahitaji hatua zaidi.

Alisema hata wakitaka mabadiliko ya katiba inawezekana na ni suala la mchakato wa vikao mbali mbali kisha kura za maoni kwa wananchi zitaitishwa.

Suala la SUK si la chama chochote cha siasa ni la kikatiba hawezi kubadili Rais Dkt. Mwinyi wala vikao vinavyoendelea" alisema na kuongeza kuwa wananchi wanasubiri kuhudumiwa na waliowachagua wakiwemo hao wa ACT Wazalendo wanaochelewa kujiunga kuunda serikali.


Mazungumzo yanayofanyika sasa yanawahusisha Rais wastaafu, Dkt. Ali Mohamed Shein na Amani Abeid Karume na ACT inawakilishwa na Mwenyekiti OMO na Juma Duni Haji.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA