CCM: SERIKALI YA UMÒJA WA KITAIFA ZANZIBAR IPO KWA MUJIBU WA KATIBA


                                              Na Mwendishi Wetu, Zanzibar

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimebainbisha kuwa suala Serikali ya Umoja wa Kitaifa lipo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na sio matakwa ya vyama vya siasa.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari Ofisi Kuu Kisiwandui, 03 Februari 2026, kuelekea maadhimisho ya kuzaliwa CCM ifikapo 05 Februari 2026, Katibu wa kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya   Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa inaundwa kwa taratibu zake lipo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar.

Mbeto ambaye alisema hayo kufuatia kusua sua kwa Chama cha ACT Wazalendo kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa toka baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2025, alibainisha kuwa mabadiliko hayo ndio yaliweka taratibu zake ili iondoke si matakwa ya vyama ni matakwa ya wananchi.

Mwenezi Mbeto alisema ACT kutokujiunga na serikali hiyo ni kuwanyima Uwakilishi wa watu waliowapigia kura Wawakilishi hao wa ACT Majimboni ambao nafasi zao za Uwaziri na Makamu wa Kwanza zipo wazi hadi hivi sasa.

Mbeto alibainisha kuwa ili kuikataa serikali hiyo hakuwezi kufanywa kienyeji  ili iwe inabidi wananchi wa Zanzibar wapige kura za maoni na robo tatu wakisema iondoke itaondoka na sio kwa matakwa ya vyama ila ya wananchi wa Zanzibar.

"Wananchi watatakiwa kupiga kura za maoni na robo tatu wakisema hawaitaki itaondoka lakini haitaondoka kwa vipingamizi vyovyote" alisema Mbeto na kuongeza kuwa serikali iliyopo itaendea kuwahudumia wananchi.

Mwenezi huyo alibainisha kuwa uwepo wa serikali hiyo ya mseto si suala la CCM na ACT hivyo vyama vya siasa vipende visipende lazima vifuate kwani Katiba na Sheria inasema hivyo.

"ACT wakisema sio kipaumbele chao kwa sasa itaendelea kuwepo kwani Chama cha Wananchi (CUF), kiliposusia  serikali awamu ya mwisho ya Rais mstaafu Dkt. Ali Mohamed Shein alizijaza nafasi na Serikali iliendelea kuwahudumia wananchi wake" alisema Mbeto.

Mwenezi huyo anasema kutokushiriki ACT kutakuwa na athari kwani wananchi walichagua kwa matumaini wangetaka wangeipa CCM kwa asilimia 100 lakini wakaipa asilimia 74.86 na ACT asilimia 23.22.

"Serikali haitaacha kuwahudumia watu wake, kuna muda wakikataa basi Mtendaji Mkuu wa shughuli zote za serikali (Rais), atafanya maamuzi yake kwa mujibu wa Katiba na Sheria" alisema Mbeto na kuwaomba ACT wakubali kuunda Serikali ili kuleta umoja wa kiTaifa.

Kulingana na Katiba ya Zanzibar, chama kilichoshika nafasi ya pili na kupata asilimia 10 ya kura zote, kinaunda serikali hiyo na kinatakiwa kuwasilisha majina ya Wawakilishi wao kwa ajili ya nafasi za uWaziri na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ndani ya miezi mitatu.

ACT kulingana na matokeo yaliyokipa asilimia 23.22 ya kura zote ukiacha Makamu wa Kwanza wa Rais, ACT imepata maWaziri wanne.

Wizara walizotengewa ni Wizara ya Maliasili na Malikale, Afya, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Viwanda na Biashara.

kupata nafasi ya kutoa mawaziri kulingana na asilimia kilizopata na kwa mantiki hiyo serikali ya umoja wa kiTaifa inaweza kuundwa    na vyama vitatu hadi vinne.

Katika uchaguzi mkuu uliopita 2025.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA