WAZIRI KAIRUKI: TUTAENDELEA KUTEKELEZA MAAGIZO YA SERIKALI







 Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Kairuki amewahakikishia Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Miundombinu kuwa wizara yake inaendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali kwa kuhakikisha huduma za mawasiliano na teknolojia ya habari zinapatikana kwa uhakika, usalama na gharama nafuu ili kuchochea uchumi wa Kidigitali.

Waziri Angellah Kairuki akiwa na watendaji wa wizara hiyo katika kikao cha pamoja na wajumbe kamati hiyo ya Bunge kilichofanyika 15 Januari 2026 katika Ukumbi wa Ofisi za Bunge Mjini Dodoma, wajumbe walipokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ikiwemo maendeleo ya miradi ya mawasiliano.

Pia upanuzi wa huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na mikakati ya Serikali kuimarisha huduma za mawasiliano kwa wananchi.

Wajumbe hao, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Moshi Selemani Kakoso ilikuwa katika kikao hicho ambacho ni sehemu ya majukumu ya kamati hiyo ya Bunge ya Miundombinu.

Kamati hiyo pamoja na mambo mengine ina jukumu la kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa shughuli za wizara na taasisi zake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanuni za Bunge.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA