RAIS MWINYI AHIMIZA FIDIA KWA WAKATI WANAOPISHA MRADI
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyezi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo 02 Januri 2026 ameagiza kulipwa fidia mara moja kwa watu wote wanaopisha mradi wa barabara za Ng'imbwa ili mradi uweze kukamilika kwa wakati.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Uzi Ng’mbwa, Mkoa wa Kusini Unguja pamoja na barabara zake.
Dkt. Mwinyi alisema ameagiza kuchukuliwa hatua madhubuti kuhakikisha waliopisha mradi wanalipwa kwa wakati.
Alibainisha kuwa kuchelewesha fidia kunasababisha miradi kuchelewa kukamilika.
Alisema katika hafla hiyo ambayo ni sehemu ya Shamra Shamra za Mapinduzi za Maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa wananchi pia wana wajibu wa kutoa ushirikiano ili kufanikisha mradi huo wenye thamani ya TSh.Billioni 36.
Daraja hilo litakuwa na urefu wa Km 2.2 lina uwezo wa kuhimili magari yenye uzito hadi kilo 60 na barabara yenye urefu wa Km 6.5 na inatarajiwa kuondoa changamoto ya muda mrefu ya usafiri na uchukuzi kwa wakazi wa eneo hilo.

Comments
Post a Comment