MBETO: MIAKA 200 YA 'MWARABU' ZANZIBAR MIJI SHANGANI,DARAJANI


                                       Mwandishi Wetu, Zanzibar

ZANZIBAR Visiwa vyenye historia ya kipekee ukanda wa Afrika Mashariki licha ya kutawaliwa na Ureno karne ya 14 baadae ukawa chini ya utawala wa kisultani wa Waarabu kutoka Oman kwa miaka 200 lakini Mji wa Zanzibar ulianzia Shangani ukaishia Darajani kutokana na watawala hao kutojali hali za wenyeji  waAfrika maskini.

Akizungumza katika mahojiano na Bahari FM mjinj Unguja leo 15 Januari 2026, Katibu wa Kamati Maalum NEC, Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema Zanzibar imetawaliwa miaka 200 na Sultan wa Oman barabara iliyokuwepo ni kutoka Shangani hadi Darajani lakini leo miaka 62 baada ya Mapinduzi, barabara za lami sio mijini tu bali hadi vijijini.

"Leo Zanzibar nzima miji imeungana kwa barabara za lami kuanzia Tunguu, Kizimkazi hadi Makunduchi na Miji ya Pemba pia na hiyo ni ndani ya miaka 62 baada ya Mapinduzi, lakini mwarabu ametawala miaka 200 hakuna maendeleo yaliyofanyika" alisema Mbeto.

Alisema mwenezi huyo kuwa mapinduzi yalifanyika ili huduma za msingi za jamii ziweze kupatikana ikiwemo elimu, matibabu, miundombinu na makazi bora kwa waAfrika maskini wa Zanzibar.

Alisema anachofanya Dkt. Mwinyi anatimiza azma ya mapinduzi ambayo ni kuwapatia wananchi kile walichokikosa kipindi kile cha utawala wa kisultani wa kiarabu.

Ndio maana mara tu baada ya Mapinduzi, Rais Amani Abeid Karume alitangaza huduma bure za afya, elimu na kuhakikisha kila mwaAfrika mZanzibar anapata makazi bora na kuanza kuwajengea nyumba bora za kuishi.

"Jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba za ghorofa Michenzani Rais wa Kwanza, Abeid Amani Karume aliliweka 1966" alisema Mwenezi Mbeto.

Ujenzi ukaanza na baadae anasema Mwenezi kuwa wakatokea nchi rafiki ya Ujerumani Mashariki (enzi hizo), wakajenga za Kikwajuni

Alibainisha kuwa ardhi yote ya Zanzibar ilikuwa inamilikiwa na watu wasiozidi watatu, ikagawanywa upya na kila mkazi mwenyeji alipatiwa ekari tatu kuanzisha na kuendelea na maisha.

Anabainisha kuwa hata shule zilizokuwepo ni kwa ajili ya wachache wakiwemo watoto wa kizungu, asili ya Kiarabu, Goa na Wahindi na shule kwa wananchi maskini si zaidi ya mbili.

"Waliopindua wametaka huduma bora ndio maana tunasema mapinduzi daima" alisema na kuongeza kuwa ni wajibu vijana wajitambue na kujua kiini cha Mapinduzi ya Zanzibar na kuyalinda kwa nguvu zote na kudumisha amani na wasifuate mkumbo.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA