MBETO: MAPINDUZI ZANZIBAR YAMEONDOA MATABAKA


                                               Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MAPINDUZI yaliyofanyika ya Zanzibar 1964 yametokana na wananchi walio wengi kuchoka kubaguliwa katika sekta zote za maendeleo ya kijamii na miundombinu ambazo kwa maono ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi anazifanyia marekebisho makubwa hivi sasa akiendeleza pale walipoishi watangulizi wake akiwemo Rais wa Kwanza, Hayati Abeid Amaan Karume.

Upende mwingine hila za kisiasa ambazo zilichagizwa na Uingereza ambao toka 1890 walikuwepo Zanzibar kulinda utawala wa kisultani ambao ndio uliokuwa umeshika hatamu baada ya kuwang'oa Ureno  zilichangia kwa kiasi kikubwa mapinduzi hayo kutokana ASP kunyimwa ushindi zaidi ya mara nne toka 1957 katika njia za kidemokrasia kwenye sanduku la kura.

Akizungumza Mjini Unguja 06 Januari 2026, ikiwa ni sehemu ya kilele cha miaka 62 ya Mapinduzi, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema chama cha Afro Shiraz Party  (ASP) hakikutaka kufanya mapinduzi, waliamini katika demokrasi za vyama lakini Uingereza wakaifanyia hiyana na kwa kuwa wananchi walikuwa wamechoka kubaguliwa katika sekta zote za kijamii zikiwemo afya, elimu, miundombinu, makazi na zingine, waliamua kufanya mapinduzi.

"Uchaguzi wa Juni 1061 ASP tulishinda lakini ukatokea Uasi n viongozi wa chama  chetu wakatiwa ndani na kufunguliwa kesi pia tulishinda hatukupewa" alisema Mbeto.

Mbeto alisema mwaka 1963 uchaguzi wa kutoa uhuru uliosimamiwa na Uingereza pia ASP kilishinda lakini Zanzibar Pemba People Party (ZPPP) na Zanzibar Nationality Party (ZNP) wakafanya hila na msimamizi wa uchaguzi hivyo vikaunganisha matokeo yao, hali iliyochochea mapinduzi.

Alibainisha kuwa wakati huo watu wa tabaka la chini walikuwa wakiishi katika makazi duni yasiyo na miundombinu yoyote huku wabaguzi hao wakiwa katika maghorofa ya Mji Mkongwe na maeneo mengine ya Mjini.

"Shule za watoto wa wananchi wa kawaida mathalan hapa Unguja ilikuwa tatu ambazo watoto wa Kiafrika wangeweza kusoma ambazo ni Gulioni nyingine ilikuwa Kiungani ambayo ni ya jamii ya Wakristu na Shimoni, iliyopo Mao" alisema Mbeto.

Anazitaja shule za Forodhani, Kiponda, Tumekuja kuwa zilikuwa za watoto wa kihindi, kiarabu na wazungu na upande wa matibabu, waafrika walitegemea hisani ya Daktari wa jamii ya Goa kutoka India aliyekuwa Mkunazini jirani na soko la zamani la watumwa aliyejulikana kwa jina la Kimoto.

Mwenezi Mbeto alisema hali hiyo ilichochea wananchi kufanya mapinduzi ya kuondoa utawala wa kisultani na kuanza kuijenga upya Zanzibar na kuondoa matabaka.

Mbeto alisema  ndio maana ikaja sera ya elimu, afya bila malipo ili  kuwapa hadhi wananchi na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Alisema kuwa Rais wa Kwanza Mzee Abeid Karume alianza kwa kuwajengea na nyumba za Michenzani kwa ajili ya kuwatoa walio wengi kwenye makazi duni.

Alisema WaZanzibar waafrika walikuwa wakiishi ktk vibanda duni na mifugo wakiwemo kuku na kila ghasia ya kungunj na viroboto

Mbeto alisema maendeleo yote anayoyafanya Rais Dkt. Mwinyi toka aingie madarakani miaka mitano iliyopita na sasa awamu ya pili ni kuya enzi mapinduzi kwani yalifanyika kuwaletea wananchi hali  bora za maisha katika sekta zote za kijamii, uchumi na biashara.

Alisema Rais huyo wa Nane, amefanya mapinduzi makubwa kwenye sekta zote hali ambayo inachangiwa na maono yake binafsi, hofu ya Mungu aliyo nayo, bidii na uchapakazi wake.

Comments