MBETO: MAPINDUZI ZANZIBAR NI KWA KIZAZI CHA SASA


                                             Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MAENDELEO yanayofanyika kwa vitendo Zanzibar hivi sasa ndio maana ya kauli mbiu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) isemayo 'Mapinduzi Daima'.

Akizungumza mjini Unguja wakati wa shamra shamra za kilele cha Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, 11 Januari 2026, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema waAfrika waliamua kufanya mapinduzi miaka 62 iliyopita baada ya kukosa haki zao na huduma za msingi za maendeleo na kijamii.

Mwenezi Mbeto alisema ndio maana kabla ya kilele cha maadhimisho ya siku hiyo Serikali ya Mapinduzi imekuwa na uzinduzi wa miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi na hiyo ndio maana ya 'Mapinduzi Daima'.

Alibainisha kuwa vijana wanapaswa kufahamu kuwa Mapinduzi Daima ni Maendeleo Daima kwani miaka 62 iliyopita watoto wa maskini Zanzibar walikosa elimu, hakukuwa na elimu bora kwa wote.

o

Mwenezi Mbeto anasema leo inapozinduliwa barabara maana yake miaka 62 iliyopita hakukuwa na barabara zenye hadhi hata  ya kifusi kwenye maeneo yao na walikuwa wanachonga njia wenyewe huko wanakoishi.

"Leo angalia barabara zilizojengwa" alisema na kuongeza kuwa hakukuwa na hospitali zinazotoa huduma za matibabu kwa waAfrika wa Zanzibar.

Kuhusu elimu Mbeto alisema Zanzibar haikuwa na chuo kikuu hata kimoja leo kuna Kampasi nyingi na Vyuo Vikuu vimejengwa kikiiwemo cha Sayansi ya Bahari na upande mwingine bandari zilizokuwepo zilikuwa za majahazi sio meli.

"Leo unapozungumzia mapinduzi ni pamoja na kujumlisha haya yanayofanyika sasa ambayo maana yake ni kuendeleza azma iliyosababisha mapinduzi" alisema.

Miaka 62 ya  Mapinduzi ya Zanzibar kumeshuhudiwa kujengwa shule za msingi na sekondari za kisasa za ghorofa zenye kila kinachohitajika kujifunza na kufundishia mijini na vijijini ambako hutolewa elimu bila malipo.

Huduma za afya bila malipo huku kukiwa na mamlaka ya kuhakikisha mgonjwa hakosi dawa katika hospitali zilizojengwa kila wilaya zenye vipimo vya magonjwa karibu  yote na madaktari ambao kati yao wamejengewa nyumba za kisasa zenye kila kitu ndani, eneo la hospitali.

Barabara za  lami ziliyozingatia ubora wa viwango vinavyotambulika kutoka mwanzo hadi mwisho wa Unguja kadhalika na Pemba.

Viwanja vya ndege vinayojengwa na vinavyofanyiwa upanuzi, bandari, nyumba bora za makazi kwa wananchi na huduma zingine ni sehemu ya mambo ambayo Mwenezi Mbeto anayabainisha kuwa yana akisi kauli mbinu ya CCM ya 'Mapinduzi Daima'

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA