MAKAMU WA PILI WA RAIS ATIMIZA AHADI KIWANI
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amekabidhi trekta kwa wakazi wa Kiwani, Mkoa wa Kusini Pemba 03 Januari 2025 ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kwa wananchi wa eneo hilo.
Trekta hilo lilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Kusini Pemba, Yussuf Ali Juma katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Mauani, Kiwani.
Makamu wa Rais katika hafla hiyo iliambatana na mkutano wa hadhara kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura na kumuwezesha kushinda katika uchaguzi mkuu uliopita 29 Oktoba 2025.

Comments
Post a Comment