KiNONDONI YAPATA UWANJA WA SOKA WA KÌSASA
KAMPUNI ya simu za mkononi ya TECNO imekabidhi uwanja mpya wa kisasa wa soka uliojengwa kwa gharama ya TShMilioni 125 kwa manispaaa ya Kinondoni ikiwa ni sehemu ya Mchango wa Kampuni hiyo kwa Jamii (CSR), eneo la Minazini Kata ya Makumbusho (maarufu kwa Mapilau), Maanipaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Uwanja huo umejengwa kufuatia maombi ya uongozi wa kampuni hiyo ambao watautunza pia walipokutana na Meya wa Manispaa Kinondoni Songoro Mnyonge la kutaka eneo kwa ajili ya kujenga kiwanja kwa ajili ya vijana kufanya mazoezi na utakuwa mali ya manisapaa Kinondoni.
Mchakato wa upatikanaji wake ulifika mezani kwa Mkurugenzi Manispaa Kinondoni, Hajjat Hanifa Suleiman Hamza ambaye aliwapa uhuru wa kuchagua eneo mojawapo kati ya yale waliyopendekeza manispaa
Meya Songoro aliishukuru TECNO kwa kuunga mkono jitihda za serikali ya Rais Samia ya kukuza na kuendelezaa vipaji vya soka nchini.



Comments
Post a Comment