DKT. MWINYI: UWEKEZAJI ZAN BREED UNUFAISHE WAFUGAJI


                                              Mwandishi Wetu,, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametaka 

Mradi mkubwa wa Uwekezaji wa Shamba la Ufugaji wa Kuku wa Zan Breed Limited ambao ameuzindua leo 08 Januari, 2026 Kitope, Mkoa wa Kaskazini Unguja kuwa ni lazima uwanufaishe wafugaji wadogowadogo.

Rais Dkt. Mwinyi alisema kunufaika kwao ni kupitia upatikanaji wa elimu ya ufugaji, vifaranga bora, chakula cha kuku, huduma za chanjo pamoja na masoko ya uhakika ili kuongeza kipato na ustawi wao.


Kufikia lengo hilo ameziagiza Wizara ya Uwezeshaji na Wizara ya Kilimo kuhakikisha wafugaji wadogowadogo wanawezeshwa kupitia mikopo isiyo na riba, mafunzo ya ufugaji na masoko, na kuutumia Mradi wa Zan Breed kama msingi wa kuwawezesha wafugaji kote Zanzibar.

Alisema mradi huo wa kimkakati unaifanya Zanzibar kufanikiwa kujitegemea na kujitosheleza katika uzalishaji wa kuku, hatua itakayopunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa kuagiza kuku kutoka nje ya nchi.

Alisema mradi huo wa kimataifa, unaoonesha uwezo wa Zanzibar kuanzisha na kuendesha miradi mikubwa ya uzalishaji wa ndani. 

Rais Dkt. Mwinyi amebainisha umuhimu wa kuwepo kwa sera za kifedha na kodi zitakazolinda wawekezaji na viwanda vya ndani ili kuimarisha hakikisha wafugaji wadogowadogo wanawezeshwa kupitia mikopo isiyo na riba, mafunzo ya ufugaji na masoko, na kuutumia Mradi wa Zan Breed kama msingi wa kuwawezesha wafugaji kote Zanzibar.

Mradi huo ambao kwa mujibu wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), una mtaji wa Dola za Marekani Milioni 105, ukitarajiwa kutoa ajira zaidi ya 1,000 na uwezo wa kuzalisha kuku 800,000 kwa mwezi, sanjari na huduma za kliniki ya kuku, kiwanda cha nafaka, maabara pamoja na mfumo wa kuchakata maji,


Dkt. Mwinyi alisema mradi una umuhimu katika kukuza sekta ya mifugo na kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA