DKT. MWINYI: TUNAJENGA MIUNDOMBINU KUIFUNGUA ZANZIBAR
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ikiwemo bandari, barabara na viwanja vya ndege, lengo ni kuifungua Zanzibar kiuchumi na kuharakisha mabadiliko chanya ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa biashara yenye urefu wa kilometa 19 ya Kitope/Ndagaa/Kidimni, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi alisema ujenzi wa miundombinu ni mhimili muhimu wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuanza kutumika kwa barabara hiyo kutarahisisha usafirishaji na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo.
"Barabara pia itaongeza uzalishaji na biashara na kusaidia upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi wa Kaskazini Unguja" alisema Rais Dkt. Mwinyi.
Dkt. Mwinyi amesisitiza wananchi kuitunza miundombinu hiyo na kuepuka ujenzi holela kwenye hifadhi ya barabara na kuheshimu mipango ya matumizi ya ardhi.
Alisema ushirikiano wa wananchi ni msingi wa kuhakikisha miradi ya maendeleo inaleta manufaa ya kudumu kwa Taifa na vizazi vijavyo.

Comments
Post a Comment